.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 17 Februari 2015

MAELFU YA WATU WAKUSANYIKA KUWAKUMBUKA WAHANGA WA COPENHAGEN

Makumi ya maelfu ya watu wamekusanyika katika miji kadhaa nchini Denmark kuwakumbuka wahanga wa matukio ya mashambulizi ya silaha yaliyotokea katika Jiji la Copenhagen.

Watu waliobeba mishumaa na tochi wametumia dakika moja kukaa kimya wakati wa kuanza kwa tukio hilo la kuwakumbuka wahanga wa mashambulio Jijini Copenhagen.

Watu wawili wameuwawa na polisi watano wamejeruhiwa katika mashambulio yaliyofanyika kwenye mdahalo wa uhuru wa kuongea pamoja na kwenye hekalu. Mtu aliyehusika na tukio hilo naye alipigwa risasi na kufa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni