.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 18 Februari 2015

RED ARROWS KUJIPIMA NA KILUVYA UNITED, RUVU SHOOTING

Timu ya Red Arrows inayoshiriki Ligi Kuu nchini Zambia, kesho siku ya alhamis itashuka uwanja wa Karume kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Kiluvya United inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL) Tanzania bara.

Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya maandalizi ya timu hiyo kutoka nchini Zambia ambayo imeweka kambi jijini Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu nchini Zambia.

Mara baada ya mchezo huo, Kikosi cha Red Arrows kitaendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Karume na Ufukwe wa Mbalamwezi kulingana na ratiba ya kocha wa timu hiyo.

Red Arrows watacheza mchezo wao wa pili na mwisho wa kirafiki siku ya jumapili dhidi ya timu ya Ruvu Shooting inayoshiriki Ligi Kuu (VPL), mchezo ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es salaam kabla ya kumaliza ziara yao siku ya jumanne na kurejea nchini Zambia.

FAINALI DARAJA LA KWANZA KUCHEZWA JUMAPILI

Timu za African Sports ya Tanga na Mwadui FC ya Shinyanga zinatrajiwa kucheza mchezo wa fainali ya kusaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) siku ya jumapili katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

African Sports waliibuka washindi wa kwanza katika Kundi A, na Mwadui FC washindi wa kwanza Kundi B watacheza mchezo huo wa fainali ambapo Bingwa atapewa zawadi ya Kombe na medali, hali kadhalika kwa msindi wa pili.

Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ilimalizika mwishoni mwa wiki kwa timu nne kupanda Ligi Kuu kwa kila kundi kutoa timu mbili, Kundi A ni African Sports na Majimaji FC, Kundi B ni timu za Mwadui FC na Toto Africans.

Nazo timu za Green Worriors na Villa Squad zimeteremka Daraja la pili baada ya kushika nafasi za mwisho kwenye msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza, Villa Squad kutoka Kundi A na Green Warriors Kundi B.

TAIFA STARS KUCHEZA NA KOMBAINI YA TANGA LEO

Timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa miguu (Taifa Stars Maboresho) leo inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya kombani ya jiji la Tanga katika Uwanja wa Mkwakwani.

Mchezo huo wa kujipima nguvu ni sehemu ya program ya kocha mkuu Mart Nooj ya kupata nafasi ya kuona maendeleo ya wachezaji wake ambao anawaandaa kuwa wachezaji wa timu ya Taifa ya baadae.

Mara baada ya mechi ya leo jioni jijini Tanga, timu hiyo itarejea jijini Dar es salaam ili kutoa fursa kwa wachezaji kujiunga na vilabu vyao kwa ajili ya michezo inayowakabili mwishoni mwa wiki ikiwemo Ligi Kuu ya Vodacom na Fainali ya Ligi Daraja la Kwanza. 


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni