.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 1 Februari 2015

ROBIN VAN PERSIE AZINDUKIA KWA LEICESTER CITY WAKATI MAN U IKIIBUKA NA USHINDI

Mshambuliaji wa Manchester United Robin van Persie amemaliza ukame wa magoli baada ya kuifungia timu yake bao moja na kuisaidia kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Leicester City.

Van Persie alifunga bao la kwanza mnamo dakika ya 27, kabla ya Radamel Falcao kuongeza bao la pili, ambapo kapteni wa Leicester City Wes Morgan alizidi kulizamisha jahazi lake kwa kujifunga.

CHELSEA NA MANCHESTER CITY HAKUBA MBABE
Mechi baina ya Chelsea na Manchester City imeisha kwa sare ya bao 1-1, matokeo ambayo yanambeba kocha Jose Mourinho na kikosi chake kuongoza ligi kuu ya Uingereza kwa tofauti ya pointi tano.

Katika mchezo huo Loic Remy alikuwa wa kwanza kucheka na wavu, lakini David Silva alisawazisha bao hilo kabla ya mapumziko na kuisaidia Manchester City kuondoka na pointi moja katika dimba la Stamford Bridge.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni