.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 18 Februari 2015

WATU 20 WAFA KATIKA MILIPUKO KATIKA MJI WA BIU NCHINI NIGERIA

Watu 20 wamekufa kufuatia kutokea milipuko kwenye eneo la ukaguzi la jeshi katika mji wa Biu kaskazini-mashariki mwa Nigeria.

Vikosi vya jeshi katika eneo hilo vilifyatua risasi na kuwauwa wapiganaji 17 ambao inaaminika kuwa ni wa kundi la Boko Haram.

Siku ya jumanne kundi hilo la Boko Haram lilitoa video ambayo kiongozi wao Abubakar Shekau alionekana akiapa kuwa atavuruga uchaguzi usifanyike kwa gharama yotoye ile.

Video hiyo ya dakika 15 ilitolewa kupitia akaunti yao ya twitta, jambo ambalo baadhi ya wachambuzi wanahisi kundi hilo limeshawishika kuwa na akunti hiyo na kundi la Dola ya Kiislam (IS).

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni