Modo Amber Rose na aliyekuwa mumewe
Wiz Khalifa wameafikiana kupatana kuhusiana na mvutano waliokuwa nao
wa kudai haki ya kumlea mtoto wao wa kiume Sebastian.
Wawili hao walikuwa wakipambana
kuhusiana na mtoto wao wa miaka miwili, huku kila mmoja akidai
mwenzake ni mzazi mbaya, lakini sasa wamebadili msimamo.
Taarifa zinadai kuwa Amber amebadili
msimamo wake baada ya kusikiliza wimbo ambao Wiz ameutunga maalum kwa
Amber uitwao See You Again.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni