.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 5 Machi 2015

BALOZI WA MAREKANI KOREA KUSINI ASHAMBULIWA KWA KISU JIJINI SEOUL

Balozi wa Marekani nchini Korea Kusini, Mark Lippert, amejeruhiwa kwa kisu baada ya kushambuliwa na mtu mmoja Jijini Seoul.

Bw. Lippert alikuwa amehudhuria mkutano wa kifungua kinywa wakati alipovamiwa na kukatwa na kisu usoni na kwenye mkono wake wa kushoto.

Balozi huyo alikimbizwa hospitali kwa matibabu, na imeelezwa kuwa majeraha yake ni madogo na hayatishii uhai wake.

Mashahidi wamesema mshambuliaji huyo mwanaume, ambaye aliwahikuwa mwanajeshi wa taifa la Korea, alipaza sauti akidai Korea Kaskazini na Korea Kusini ziunganishwe.
         Matone ya damu yakiwa yamedondokea kwenye meza aliyokaa balozi huyo 
                                   Maafisa usalama wakiwa wamemdhibiti mvamizi huyo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni