Bodi ya marefa wa kulipwa imesema
adhabu ya kutolewa kwa kadi nyekundu beki ya Sunderland Wes Brown
katika mchezo wa jana dhidi ya Manchester United si tukio la refa
kushindwa kumbaini muhusika.
Refa Roger East alimtoa Brown, kwa
kile kinachoonekani ni kwa makosa katika mchezo ambao Manchester
United iliibuka nyumbani na ushindi wa mabao 2-0.
Katika tukio hilo picha za
televisheni zinaonyesha John O'Shea akimfanyia madhambi mshambuliaji
wa Manchester United Radamel Falcao, lakini kadi akapewa Wes Brown.
Hata hivyo Mafisa wa Chama cha
Marefa wa Kulipwa Uingereza , wamesema refa East anadhani Brown ndie
amemfanyia madhambi Falcao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni