Kiongozi wazamani wa Singapore, Lee
Kuan Yew, ambaye aliibadilisha nchi hiyo kutoka mji wa bandari na
kuwa taifa lenye uchumi mkubwa duniani amefariki dunia akiwa na umri
wa miaka 91.
Waziri huyo mkuu wa taifa hilo kwa
miaka 31, alikuwa akiheshimiwa mno kama mratibu wa maendeleo ya
Singapore.
Hata hivyo alikosolewa kwa kuongoza
kwa mkono wa chuma, ambapo wakati wa utawala wake uhuru wa kutoa
maoni ulibanwa huku wapinzani wa kisiasa walikuwa wakifikishwa
mahakamani.
Maziko ya kitaifa ya Lee Kuan Yew,
yatafanyika machi 29, baada ya wiki moja ya kuomboleza.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni