Kiungo wa Manchester United Marouane
Fellaini jana usiku aliifungia magoli mawili timu yake ya taifa ya
Ubelgiji wakati ikiibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Cyprus,
katika mchezo wa kuwania kucheza michuano ya mabigwa wa bara la
Ulaya.
Katika
mchezo huo Fellaini alifunga goli la kwanza mnamo dakika ya 21, kabla
ya Christian Benteke kupachika la pili dakika ya 35 kufuatia pande
kali kutoka kwa kiungo wa Chelsea Eden Hazard.
Benteke akipongezwa na wenzake baada ya kupachika bao.
Wakati
huo huo kiungo wa Arsenal, Aaron Ramsey pamoja na winga wa Real
Madrid, Gareth Bale waliweza kuiongoza vyema timu ya taifa ya Wales
kuwafunga wenyeji Israeli kwa mabao 3-0 katika mchezo mwingine wa
kuwania kucheza michuano ya mabigwa wa bara la Ulaya.
Katika
mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Ofer mjini Haifa, Bale
alimtengenezea bao Ramsey katika kipindi cha kwanza kabla na yeye
kucheka na nyavu mara mbili katika kipindi cha pili.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni