Ndege ya shirika la ndege la Canada
imepitiliza njia ya kutulia wakati ikitua kwenye uwanja wa ndege wa
Halifax.
Abiria wote 132 waliokuwa kwenye
ndege hiyo aina ya A320 Airbus waliondolewa kwenye ndege miongoni
mwao 22 wamepelekwa hospitali kwa matibabu baada ya kupata majeraha
madogo.
Ndege hiyo namba AC624 ikitokea
Toronto iliwasili katika uwanja huo usiku wa manane na imeripotiwa
kuwa iligonga nguzo ya umeme baada ya kutua.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni