Bondia Kell Brook amerejea ulingoni
kwa ushindi baada ya tukio la kushambuliwa kwa kisu mwaka jana na
kutetea taji lake la dunia la IBF uzito wa welterweight kwa staili
yake.
Brook ambaye anarekodi ya kutupigwa
alimpeleka chini mpinzani wake Jo Jo Dan mara nne katika mchezo
ulioishia kwa KO katika raundi ya nne.
Kwa ushindi huo Brook sasa
anatarajiwa kupata pambano lenye fedha nyingi dhidi ya mabondia
Juan Manuel Marquez, Marcos Maidana
ama Amir Khan.
Jo Jo Dan akienda chini baada ya kupigwa konde la kushoto na Brook.
Jo Jo Dan chini tena hapa ilikuwa ni ngumi nzito ya kulia.
Brook hakuwa na huruma kwa Jo Jo Dan ambaye alijikuta sakafuni tena.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni