Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe na Mbunge wa Viti Maalum,
Al Shaymar Kweigyr wakiongoza matembezi ya hamasa ya kupiga vita
mauaji ya albino nchini yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam
kuanzia viwanja vya Biafra mpaka Leaders Club, Kinondoni jijini Dar
es Salaam.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, Mbunge wa Viti Maalum, Al
Shaymar Kweigyr, Balozi wa Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu,
Mwakilishi wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Abdillah Omar
sambamaba na wadau wengine wakishiriki kuimba wimbo 'Tanzania
Tanzania' kabla ya kuanza kwa shughuli nzima ya hamasa ya kupiga vita
mauaji ya albino nchini, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders
Club, jijini Dar es salaam.
Mbunge
wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr akicheza muziki wa sambamba na
Mwanamuziki wa Reggae,Jhiko Manyika "Jhikoman" wakati wa
shughuli nzima ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini,
iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es
salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network ambao ni
wadau wakubwa wa harakati ya Imetosha, Joachim Mushi.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya Matembezi ya Hamasa ya kupiga vita mauaji
ya albino nchini (Imetosha), Ally Masoud "Kipanya"
akimkaribisha Balozi wa Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu ili
kuzungumza na Watanzania waliofika kwenye Viwanja vya Leaders Club,
Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni