Vinara wa ligi kuu nchini Uingereza, Chelsea jana walinusurika kipigo toka kwa Hull City katika mchezo wa ligi kuu nchini humo, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.
Katika mchezo huo, Chelsea walianza mpira kwa kasi na kulisakama kwa nguvu lango la Hull na kufanikiwa kupata mabao mawili ya haraka haraka toka kwa Eden Hazrd katika dakika ya pili ya mchezo na Diego Costa akifunga bao la pili katika dakika ya tisa ya mchezo.
Hata hivyo mambo yalibadilika dakika chache baada ya Hull kuzinduka na kujibu mapigo na kufanikiwa kusawazisha mabao yote mawili, baada ya Ahmed Elmohamady kufunga bao katika dakika ya 26 na dakika mbili baadaye, dakika ya 28 Abel Hernandez akafunga bao la pili, hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa zimefungana mabao 2-2.
Mtokea benchi, Loic Remmy aliinusuru Chelsea na sare baada ya kufunga bao la 3 katika dakika 77 na hivyo kuifanya timu hiyo kufikisha pointi 67.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni