Askari polisi wawili wamefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi katika tukio lililotokea jana usiku katika kizuizi cha barabarani eneo la Kipara Mpakani, wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa, polisi hao wakiwa katika kizuizi hicho, watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliwavamia ghafla na kuanza kuwashambulia na hatimaye kufanikiwa kupora bunduki moja aina ya SMG na baadaye kutokomea nayo kusikojulikana.
Mbali ya kuuawa kwa polisi hao wawili, pia askari polisi mwingine mmoja amejeruhiwa huku mwingine akifanikiwa kukimbia baada ya kuzidiwa nguvu wakati akijaribu kuwanusuru askari wenzake.
Tutawaletea taarifa zaidi baadaye. Picha tulizozipata kutoka eneo la tukio hatuwezi kuweka hapa.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni