Kaburi la kiongozi wa Irak
alinyeng'olewa madarakani Saddam Hussein limebomolewa na kusawazishwa
kabisa kufuatia mapigano yanayoendelea karibu na mji wa Tikrit.
Picha zilizopigwa na shirika la
habari la AP, zinaonyesha kilichobakia katika kaburi hilo la kifahari
ni nguzo ambazo zilikiuwa zikishikilia paa la jengo la kaburi.
Vikosi vya jeshi la Irak wapiganaji
wa Shia wanaoungwa mkono na Iran wanapigana kuwaondoa wapiganaji wa
kundi la Dola ya Kiislama (IS) huko Tikrit.
Mwaka uliopita jamii ya wasuni
walisema wameuondoa mwili wa Saddam, na kwenda kuuzika katika eneo
ambalo halijulikani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni