Wanawake na watoto ni miongoni mwa
makumi ya watu waliokufa katika uvamizi uliofanyika kwenye kijiji
kimoja kilichopo kati kati ya Nigeria.
Polisi wamesema watu 45 wamekufa
katika shambulio hilo lililofanywa na watu wenye silaha katika kijiji
cha Egba kwenye jimbo la Benue.
Mmoja wa wanasiasa wa eneo hilo Audu
Sule amesema wanakijiji 81 wameuawa na wavamizi hao ambao wote
walikuwa na silaha aina ya Kalashnikov.
Mapambano baina ya wafugaji wa
kabila la Fulani na wakulima kugombani maeneo ya kuchungia mifugo
yameutumbukiza mkoa huo kwenye machafuko.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni