Waziri wa Afrika Kusini Collins
Chabane pamoja na maafisa wake wawili wa ulinzi wamekufa katika ajali
ya gari.
Gari la waziri huyo wa Utumishi wa
Umma liligongana na lori kaskazini mashariki mwa mji wa Polokwane.
Chabane, mwenye umri wa miaka 54,
pia mjumbe wa Kamati Kuu ya chama cha ANC na rafiki wa karibu wa Rais
Jacob Zuma. Pia ndiye aliyesimamia maandalizi ya maziko ya Mzee
Nelson Mandela.
Rais Zuma amesema ameshtushwa mno na
ajali hiyo iliyokatisha maisha ya rafiki yake na kuongeza kuwa kifo
hicho ni pengo kubwa kwa serikali na taifa zima kwa ujumla.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni