Mashirika ya ndege duniani yameanza
kutaka marubani wawili kuwapo muda wote katika chumba cha kurushia
ndege kufuatia tukio la ajali ya ndege katika Mlima Alps nchini
Ufaransa.
Mashirika makubwa ya ndege ya
Canada, Norway, Ujerumani pamoja na Uingereza yameahidi kubadili sera
zao.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya
Uingereza (CAA) imesema itafuatilia matokeo ya uchunguzi wa ndege
Germanairwings, kufuatia kuwepo za taarifa za rubani kuiangusha ndege
hiyo makusudi.
Shirika la ndege la Lufthansa
limesema hata kama kungekuwa na ulinzi mzuri vipi, hakuna namna
ingewezekana kumzuia rubani mwenye nia mbaya.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni