Karibu watu 19 wamejeruhiwa baada ya
kutokea mlipuko uliosababisha majengo mawili kuanguka katika Jiji la
New York.
Hadi jana mchana majira ya Marekani
zaidi ya zimamoto 200 walikuwa wakipambana na moto wa mlipuko huo,
ambao uliathiri majengo manne.
Meya wa Jiji la New York, Bill de
Blasio amesema hakuna ripoti ya mtu aliyepotea, hata hivyo amekiri
hali ni tete.
Maafisa wa Jiji hilo wanaamini
kulikuwa na kazi ikiendelea katika majengo hayo yenye mfumo wa gesi
kabla ya kulipuka.
Vikosi vya zimamoto vikipambana na moto
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni