Katibu Mkuu wa Chama tawala cha NRM,
Justine Kasule Lumumba, amesema jumla ya wabunge 80 wa NRM nchini
Uganda wamegeuza magari yao kuwa ofisi kutokana na ukosefu wa nafasi
za ofisi bungeni.
Bw. Lumumba amesema matatizo hayo ni
miongoni mwa changamoto kadhaa zinazowakabili wabunge zikiwemo kubeba
mizigo ya kuwalipia ada watoto wa wapiga kura wao, kutatua kero za
majimbo yao na kujikuta wakidaiwa na mabenki na kushindwa kulipa.
Lumumba amesema wakati wa kipindi
chake cha Unadhimu Mkuu wa Bunge, alikuwa anakabiliwa na changamoto
ya kuwataka wabunge kutoka kwenye magari yao wakifanyakazi za ofisi,
ili warejee bungeni kwenye vikao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni