Mchezaji wa Manchester United ambaye
anasugua benchi Radamel Falcao ametuma ujumbe kwa kocha wake Louis
van Gaal baada ya kufunga magoli mawili ya kiufundi kwa timu yake ya
taifa ya Colombia katika mchezo wa kirafiki na Bahrain, jana usiku.
Falcao aliyafunga mabao hao mawili
ndani ya dakika nne, yakiwe ni mabao ya Colombia ya tatu na la nne,
katika ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya taifa la Bahrain linaloshika
nafasi ya 103 katika msimamo wa Fifa duniani.
Falcao mwenye umri wa miaka 29
amekuwa aanzishwi katika kikosi cha kwanza na Manchester United tangu
Februari 28, lakini ameweza kutekeleza wajibu wake kwa timu ya taifa
kwa mujibu wa kocha wao Jose Pekerman.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni