Mawaziri kutoka nchi sita zenye
nguvu duniani wanatarajiwa kukutana hii leo kwa siku nzima na waziri
wa mambo ya nje wa Iran kuhusiana na mpango wake wa kurutubisha
nishati ya nyuklia.
Siku ya mwisho ya kufikia
makubaliano ya Iran kusitisha mpango huo, imepangwa kuwa ni jumanne.
Lengo la makubaliano hayo ni
kuifanya Iran, kuwa mwaka mmoja nyuma kabla ya kuweza kutengeneza
mafuta ya kutosha ya nyuklia yatakayoiwezesha kutengeneza silaha ya
nyuklia.
Wawakilishi kutoka Marekani,
Ujerumani, Ufaransa, Uingereza na Urusi wanashiriki mazungumzo hayo
yanayofanyika katika Jiji la Lausanne nchini Switzerland.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni