Zoezi la kuhesabu kura nchini
Nigeria linaendelea huku rais aliyemadarakani Goodluck Jonathan
akikabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa kiongozi wa zamani wa
kijeshi Muhammadu Buhari.
Tume ya uchaguzi ya Nigeria imesema
kuwa inatarajia kumtangaza mshindi wa urais hii leo, katika uchaguzi
huo ambao wapigakura walipiga kura kwa siku mbili kutokana na
hitilafu.
Umoja wa Mataifa umepongeza uchaguzi
huo licha ya kuwepo kwa hitilafu za kiufundi, maandamano ya kupinga
na vurugu zinazohusishwa na kundi la Boko Haram.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni