Mazungumzo ya kufikia makubaliano
kuhusu progamu ya nyuklia ya Iran yanaingia katika siku ya mwisho.
Mawaziri wa nchi za nje kutoka
katika mataifa manne yenye nguvu duniani pamoja na mwenzao wa Iran
wamekuwa wakijadiliana nchini Switzerland kabla ya siku ya mwisho ya
mazungumzo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani
John Kerry amesema mazungumzo ya jumatatu yameonyesha ishara nzuri,
lakini masuala muhimu bado.
Mawaziri hao wanataka Iran kuachana
na mpango wake wa kurutubisha nyuklia, ili iweze kuondolewa vikwazo
vya kiuchumi iliyowekewa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni