Mkurugenzi Msaidizi wa Mashtaka
ambaye alikuwa akiongoza upande wa mashtaka katika kesi ya tukio la
ugaidi la Jijini Kampala lililotokea Julai 2010 nchini Uganda
ameuwawa jana jioni.
Polisi wamesema Joan Kagezi aliuwawa
majira ya saa mbili usiku na watu wenye silaha waliokuwa wakiendesha
pikipiki katika eneo la Kiwatule lililopo nje kidogo ya Jiji la
Kampala wakati akirejea nyumbani.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Upelelezi Grace Akullo, ambaye alienda sehemu ya tukio, amethibitisha
tukio hilo ambapo amesema mwili wa Kagezi umehifadhiwa kwenye
hspitali ya Mulago, na uchunguzi wa mauaji yake unaendelea.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni