Rais Barack Obama wa Marekani
anatarajiwa kuitembelea Kenya kwa mara ya kwanza tangu awe rais
katika ziara yake aliyopanga kuifanya mwezi Julai, mwaka huu na
atakuwa rais wa kwanza wa taifa hilo aliyepo madarakani kutembelea
Kenya.
Rais Obama mwenye asili ya Kenya,
anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa wa dunia wa Ujasiriamali wa mwaka
2015 Jijini Nairobi, ambao unaandaliwa kwa ushirikiano baina ya Kenya
na Marekani.
Msemaji wa Ikulu ya Kenya Manoah
Esipisu ametangaza ujio huo wa rais Obama jana mara tu baada ya Ikulu
ya Marekani kuthibitisha ziara hiyo, ambayo inahusiana na tukio hilo
la mkutano huo wa kila mwaka wa dunia ambao umekuwa ukifanyika tangu
mwaka 2009.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni