Marehemu AK47 kushoto akiwa na kaka yake Jose Chameleone
Mdogo wa kiume wa msanii wa muziki
Jose Chameleone, Emmanuela Mayanja Hammertone maarufu zaidi kama
AK47, amefrariki dunia usiku wa jana baada ya kuanguka ghafla akiwa
chooni katika pub maarufu ya Dejavu nchini Uganda.
Mwili wa AK47 uligundulika majira ya
saa 2 usiku na kukimbizwa katika hospitali ya Nsambya na baadae
kuthibitishwa kuwa tayari amekwishapoteza maisha na zoezi la kuuaga
mwili wa marehemu linafanyika leo katika jengo la National Theater.
Salamu za rambirambi zimeendelea
kumiminika kwa familia ya Mayanja kufuatia taarifa za msiba huo
mzito.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni