Wabunge wa Kenya watachunguza
kitendo cha shirika la taifa la ndege Kenya kukataa ombi la Rais
Yoweri Museveni wa Uganda la kumsafirisha kutoka Uganda kwenda Jijini
Nairobi nchini Kenya.
Mbunge Ndung'u Gethenji amesema
kunahaja ya kufanyika kwa uchunguzi juu ya kitendo hicho kinachoweza
kuitia aibu Kenya.
Shirika la Kenya Airways lilikataa
ombi la Rais Yoweri Museveni kumchukua akiwa nyumbani kwao Magharibi
mwa Uganda Februari 20, mwaka huu. Shirika hilo tayari limesema
linajutia kitendo hicho.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni