Mgombea wa chama kikuu cha upinzani
nchini Kenya cha ODM, jana usiku ametangazwa kuwa mshindi katika
uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Kajiado ya Kati uliokuwa na ushindani
mkubwa.
Mgombea huyo Elijah Memusi amepata
kura 16,008 na kumshinda mgombea wa chama cha JAP Patrick Tutui
aliyeibuka wa pili kwa kupata kura 15,508 huku mgombea binafsi Kuntai
Nkashuma akiibuka watatu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni