Nchi ya Liberia imethibitisha kuwepo
tukio jipya la mgonjwa wa Ebola, na kuathiri matumaini ya nchi hiyo
kutangazwa hivi karibuni kutokuwa kabisa na mlipuko wa ugonjwa huo
hatari.
Kulikuwa hakuna taarifa za kuwepo
kwa mgonjwa mpya wa Ebola kwa siku 20 nchini humo, kabla ya mwanamke
mmoja kubainika kuwa na virusi vya ugonjwa huo siku ya Ijumaa, katika
Jiji la Monrovia.
Shirika la Afya Duniani (WHO)
huhitaji siku 42 baada ya mgonjwa wa mwisho wa Ebola kupona ili
kuweza kuitangaza nchi husika kuwa ipo salama dhidi ya maambukizi ya
Ebola.
Ugonjwa wa Ebola umeuwa watu zaidi
ya 4,000 nchini Liberia tangu kuibuka kwa mlipuko wake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni