Mshambuliaji wa tatu bado
anavikimbia vyombo vya dola, baada ya shambulio baya kwenye jumba la
Makumbusho la Bardo nchini Tunisia, lililouwa watu 25.
Rais wa Tunisia Beji Caid Essebsi
amesema licha ya kuuwawa kwa washambuliaji wawili bado kuna mtu wa
tatu ambaye bado anatafutwa na vyombo vya dola na kuahidi hatafika
mbali kabla ya kutiwa nguvuni.
Watuhumiwa kadhaa wamekamatwa kwa
kuhusika na shambulio hilo, ambalo washambulia wawili tu ndio
wanahisiwa kuhusika na shambulio hilo katika jengo la makumbusho ya
taifa hilo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni