Mcheza tenesi namba moja duniani
Novak Djokovic amepata ushindi mwepesi wa sita dhidi ya Andy Murray
na kutinga fainali za michuano ya BNP Paribas, huko Indian Wells.
Bingwa huyo mtetezi alimnyong'onyeza
mchezaji tenesi namba moja Uingereza mara tatu katika seti ya kwanza
na katika seti ya pili na kuibuka mshindi kwa seti 6-2 6-3 katika
muda wa dakika 88.
Kwa ushindi huo Djokovic atakutana
na Roger Federer katika mchezo wa fainali utakaochezwa hii leo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni