.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 22 Machi 2015

WIZARA YA ULINZI YA MAREKANI YAFUATILIA TISHIO LA IS DHIDI YA WANAJESHI WAKE

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema kuwa inachunguza tishio la njia ya mtandao linalodaiwa kufanywa na kundi la Dola ya Kiislam (IS) dhidi ya wanajeshi wake wapatao 100.

Orodha ya majina ya wanajeshi hao pamoja na anuwani zao zimewekwa kwenye tovuti inayohusishwa na IS, na kutolewa wito wa wanajeshi hao wauwawe.

Kundi hilo limesema limepata taarifa za wanajeshi hao baada ya kufanya udukuzi kwenye seva na data za maafisa wa Marekani.

Vyanzo vya usalama vya Marekani, vimenukuliwa vikisema wanajeshi waliotajwa wameshapatiwa taarifa ili kuchukua tahadhari.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni