Rais wa Guinea, Alpha Conde
ametangaza siku 45 za dharura za kiafya, katika mikoa mitano
magharibi na kusini magharibi mwa nchi hiyo kutokana na mlipuko wa
Ebola.
Tahadhari hiyo ni pamoja na kuweka
karantini kwa hospitali na zahanati ambazo mlipuko mpya wa ugonjwa wa
Ebola umebainika, pamoja na taratibu mpya za maziko na kuzuia watu
kutoka ndani ya nyumba zao.
Mlipuko wa Ebola ulianza Guinea
mwezi Desemba mwaka 2013, ambapo Januari mwaka huu Shirika la Afya
Duniani liliripoti kushuka mno kwa matukio ya watu wanaougua Ebola
nchini humo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni