.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 30 Machi 2015

RAIS WA ZANZIBAR, DK. SHEIN AWAANDALIA CHAKULA VIJANA WA HALAIKI NA VIKOSI VYA ULINZI

1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiweka chakula alichowaandalia Askari wa Vikosi vya Ulinzi Zanzibar vilivyoshiriki katika sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hafla hiyo ilifanyika jana katika kambi ya JWTZ Migombani Wilaya ya Magharibi Unguja (kulia) Mkuu wa Kikosi cha 101 Kj Zanzibar Brigedia Generali.
2
Baadhi ya Viongozi mbali mbali waliolikwa katika chakula kilichowaandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa Askari wa Vikosi vya Ulinzi Zanzibar vilivyoshiriki katika sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hafla hiyo ilifanyika jana katika kambi ya JWTZ Migombani Wilaya ya Magharibi Unguja.
3
Kamishna wa Kikosi cha Zima Moto Zanzibar Ali Abdalla Maalim Ussi akiagana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein baada ya kumalizika hafla ya chakula cha mchana kwa Askari vikosi vya Ulinzi vilivyoshiriki katika sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar haflailiyofanyika kambi ya JWTZ Migombani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,
4
Makamanda wa vikosi mbali mbali vya Ulinzi Zanzibar wakiwa katika sherehe ya Chakulacha mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa vikosi hivyo vilivyoshiriki katika sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hafla hiyo ilifanyika jana katika kambi ya JWTZ Migombani Wilaya ya Magharibi Unguja.
5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkuu wa Kikosi cha JWTZ 101 Kj Zanzibar Brigedia Generali Muhaiki baada ya kumalizika kwa hafla ya chakula kilichoandaliwa kwa Askari wa Vikosi vya Ulinzi Zanzibar vilivyoshiriki katika sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar jana katika kambi ya JWTZ Migombani Wilaya ya Magharibi Unguja.
6
Baadhi ya Vijana walioshiriki katika halaiki ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakichukua Chakula katika hafla ya iliyoandaliwa kwa ajili yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo
8
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) mara alipowasili katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo katika sherehe za hafla ya chakula maalum kwa Vijana walioshiriki Halaiki ya sherehe za Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
9
Baadhi ya Vijana walioshiriki Halaiki ya sherehe za Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakiwa katika hafla ya chakula maalum iliyoandaliwa kwa ajili yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo
10
Hawa ni miongoni mwa Vijana walioshiriki katika halaiki ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakiwa katika hafla ya chakula kilichondaliwa kwa ajili yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja leo
11
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitia chakula wakati wa hafla maalum ya chakula aliyowaandalia Vijana walioshiriki katika Halaiki ya sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar iliyofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.
13 14
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Viongozi waliohudhuria katika hafla ya chakula kilichoandaliwa kwa Vijana walioshiriki Halaiki katika Sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hafla hiyo ilifanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja.

                                                                                               [Picha na Ikulu.]

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni