Balozi wa Taasisi ya Imetosha ambaye pia ndiye mwanzilishi wa Taasisi hiyo, Henry Mdimu akitoa hotuba yake fupi kwa mgeni rasmi pamoja na mamia ya washiriki (hawapo pichani) wa matembezi ya hisani ambayo yaliandaliwa na taasisi hiyo ikiwa ni Kampeni Maalum ya kupinga mauaji ya albino nchini. Kwa mujibu wa Mdimu, taasisi yake inatarajia kwenda katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kutoa elimu kwa wananchi hao kuhusiana na imani potofu dhidi ya mauaji ya albino. Sehemu ya washiriki wa Matembezi ya Hisani ya kupinga mauaji ya albino nchini wakifanya mazoezi ya viungo baada ya kufanya matembezi hayo yaliyoandaliwa na Viongozi na Wanaharakati wa Taasisi ya Imetosha inayopambana na kutokomeza mauaji ya watu wenye ualbino nchini. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani), aliyaongoza matembezi hayo yaliyoanzia viwanja vya Biafra na kuishia viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam na kuwaomba wananchi washirikiane na Serikali kuwalinda watu wenye ualbino ili kusambaratisha mauaji hayo ambayo yanaendelea nchini.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni