Nchi ya Switzerland itarejesha
nchini Nigeria kiasi cha dola milioni 380 zinazodaiwa kuibiwa na
aliyekuwa kiongozi wa kijeshi wa taifa hilo Sani Abacha.
Urejeshaji wa fedha hizo utafanyika
chini ya usimamizi wa Benki ya Dunia, utamaliza kesi iliyodumu kwa
miaka 16 dhidi ya familia ya Sani Abacha.
Nchi ya Switzerland tayari
ilisharudisha dola milioni 700, kufuatia ombi la Nigeria. Abacha
aliongoza taifa hilo la Afrika Magharibi kibabe tangu mwaka 1993 hadi
mwaka 1998.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni