Waziri Mkuu wa Israel Benjamin
Netanyahu wa chama cha mrengo wa kulia cha Likud amepata ushindi wa
kushangaza katika uchaguzi wa nchi hiyo uliofanyika jana.
Matokeo ya awali yameonyesha kufanya
vibaya kwa chama cha Umoja wa Kizayuni chenye kufuata mrengo wa
kushoto wa kati.
Huku kura nyingi zikiwa
zimehesabiwa, chama cha Likud kinasemekana kimeshinda viti 29 kati ya
viti 120 vya bunge huku Umoja wa Chama cha Kizayuni ukipata viti 24.
Iwapo ushindi huo utathibitishwa hii
inamaanisha uwezekano wa kuundwa kwa serikali ya muungano na vyama
vingine itakayoongozwa na Bw. Netanyahu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni