Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini
jana amenusurika katika zoezi la bunge kumpigia kura ya kutokuwa na
imani naye.
Hoja hiyo ililetwa bungeni na mbunge
wa chama cha upinzani cha DA, Mmusi Maimane, iligonga mwamba baada ya
wabunge wengi wa chama tawala cha ANC kuipinga.
Jumla ya kura 221 zilipinga hoja
hiyo, huku kura 113 zikiunga mkono, katika zoezi la upigaji kura
lililolazimika kuchelewa kwa muda baada ya kubaini mfumo wa kupigia
kura wa kielektroniki kushindwa kufanya kazi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni