Baba wa msanii Emmanuel Mayanja
Hummertone maarufu kama AK47, Mzee Gerald Mayanja amesema anataka
majibu kuhusu nini kimemuua mtoto wake huyo na kuwaomba polisi
kuharakisha uchunguzi wa kifo chake.
Mzee Mayanja ametoa kauli hiyo huko
maziko ya mwanae AK47 yakipangwa kufanyika kesho huko Mityana, ambapo
mwili wake uliwekwa jana jioni katika eneo la National Theatre kwa
ajili ya watu mbalimbali kutoa heshima zao za mwisho.
Watu wengi walijitokeza jana
National Theatre kuungana na familia ya Mzee Mayanja katika
kuomboleza kifo cha ghafla cha AK47, ambapo huzuni zilitawala katika
eneo lote la viwanja vya National Theatre.
Emmanuel Mayanja ambaye ni mdogo wa
msanii nyota wa Uganda Jose Chameleone alitangazwa kufariki dunia
katika hospitali ya Nsambya, baada ya kudaiwa kuanguka akiwa chooni
kwenye klabu ya DEJAVU iliyopo Kansanga.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni