Matokeo ya utafiti uliofanywa kwa
muda mrefu umeonyesha uwepo wa uhusiano baina ya unyonyeshaji maziwa
ya mama watoto na uwezo wao wa kiakili.
Utafiti huo uliofanywa nchini Brazil
kwa kuhusisha watoto wapatao 3,500 wa maisha tofauti, umebaini watoto
walionyonyeshwa kwa muda mrefu walipata alama za juu katika mtihani
wa kupima uwezo wa akili zao.
Wataalam hao wanasema matokeo hayo
ambayo si ya mwisho, yanaonekana kuunga mkono ushauri unaotolewa wa
watoto wachanga wanapaswa kunyonyeshwa maziwa ya mama tu kwa kipindi
cha miezi sita.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni