.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 28 Machi 2015

UCHAGUZI MKUU NIGERIA, WANANCHI KUAMUA NI GOODLUCK JONATHAN TENA AU MUHAMMADU BUHARI

Wananchi nchini Nigeria leo wanapiga kura kumchagua rais atakayeliongoza  taifa hilo kubwa barani Afrika, katika uchaguzi ambao bado unatishiwa na kundi la kigaidi la Boko Haramu ambalo limekuwa likifanya mauji ya raia na utekaji wa watu nchini humo. 

Uchaguzi wa leo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali, kwani Rais Goodluck Jonathan toka chama cha People's Democratic Party (PDP) anayewania muhula mwingine wa kuliongoza taifa hilo, anakabiliwa na upinzani mkubwa toka kwa hasimu wake Muhammadu Buhari wa chama cha All Progressives Congress (APC). 

Mataifa mbalimbali yameitaka Nigeria kufanya uchaguzi wake katika hali ya amanio na utulivu, huku serikali yenyewe ya Nigeria ikiwahakikishia wananchi wake usalama na kuondokana na hofu ya mashambulio toka Boko Haramu kwani ulinzi utaimarishwa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni