Jeshi la polisi mkoani Geita
linawashilikilia waganga wa kienyeji 32 kwa kupiga ramli chonganishi,
ambao wamekutwa na zana zao za kufanyia udangayifu zikiwemo nyara za
serikali za wanyama tofauti wakiwemo Kakakuona, Fisimaji, Nyoka
waliokaushwa, Sarafu za fedha za aina tofauti, ngozi za chui na mikia
ya nyumbu, pembe na kucha za wanyama ambavyo vyote huvitumia kupigia
ramli chonganishi.
Aidha, waganga hao wanadaiwa
kuendesha upigaji ramli ikiwemo kuwasafisha kwa kuwatoa mikosi wauaji
wa walemavu wa ngozi na vikongwe kwa kuwapa dawa za ujasiri na baada
ya kutejeleza ukatili huo waganga hao wanadaiwa kuwatengenezea tena
dawa wa kuwasafisha kwa kuwatoa mikosi vitendo vinavyodaiwa kuwa
chimbuko la mauaji ya kikatili ya kutumia mapanga kwa walemavu
wangozi na vikongwe.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita
Kamisha msaidzi mwandamizi Joseph Konyo ameyasema hayo leo katika
mkutano wake na waandishi wa habari ikiwa ni siku moja tu toka
mahakama kuu kanda ya Mwanza kuwahukumu watuhumiwa wanne wa mlemavu
wangozi adhabu ya kunyongwa ahadi kufa.
Akitoa uafafanuzi juu ya kutiwa
mbaroni kwa watuhumiwa hao Kamanda Konyo amesema waganga hao
wamekamatwa katika oporesheni ya siku mbili enedeleu ya juzi na jana
ambapo hao ni sehemu ya waganga zaidi ya 2000 wanaoendesha vitendo
hivyo vya uchonganishi na utaperi huku wilaya ya Geita peke yake
ikikadriwa na kwua nawaganga zaidi ya 900,Wilaya ya Chato waganga
400,Mbogwe waganga zaidi ya 500,Bukombe 600 na Nyang'hwale 300.
Kabla ya baadhi ya waganga kutiwa
mbaroni polisi kupitia kitengo cha Upelelezi wa makosa ya jinai na
Intelijensia waliweka mitego na kufanikiwa kuwaingiza mtegoni baadhi
ya wapiga ramli waonaodai wana uwezo wa kuwawezesha watu kupata
utajiri kwa kuchimba dhahabu na bahati ya nyota kwa biashara kwa
kuwapigia ramli hatua iliyodaiwa kuwa imekuwa chanzo na uchochezi wa
mauaji ya vikongwe na walemavu wangozi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni