.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 19 Machi 2015

WAKUTANA KUJADILIANA JINSI YA KUKABILIANA NA MAUAJI YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI

1
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Bahame Nyanduga akisoma hotuba ya kuwakaribisha wajumbe wa mkutano wa wadau katika kupanga mikakati ya namna ya kutoa elimu ya umma ili kutokomeza tatizo la mauji na ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi uliandaliwa na tume hiyo jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Iddi Mapuri.
2
Mkurungezi wa Taasisi ya Under The Same Sun Bi. Bicky Ntetema akitoa taarifa za utafiti kuhusu mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini katika mkutano ulifanyikia jijini Dar es Salaam na kushirikisha wadau mbalimbali ikiwa ni njia mojawapo ya kupanga mkakati wa namna ya kutoa elimu kwa umma katika kutokomeza tatizo la mauji na ukatili dhidi ya watu hao wenye ulemavu wa nguvu, kulia kwake ni Afisa Utetezi na Uelimishaji wa Taasisi ya Under the Same Sun Bw.Kondo Seif na kushoto ni Afisa Uhusiano na Habari wa Chama Cha Albino Tanzania Bw. Josephat Turner.
3
Mwanasheria kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw. Shadrack Makongoro akitoa ufafanuzi kuhusu sheria,wakati wa mkutano wa wadau mbalimbali katika kupanga mkakati wa namna ya kutoa elimu kwa umma katika kutokomeza tatizo la mauji na ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
4
Mwakilishi wa UNESCO nchini Bi. Zulmira Rodrigues akitioa mapendekezo ya nini kifanyike katika kudhibiti mauji na ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu nchini ambapo alipendekeza kuwa elimu kwa umma itolewa kupitia Radio za Kijamii (Community Radio) zinazowafikiwa watu wengi ili kuondokana na dhana potofu kuhusu mauji hayo.
5
Mkurungezi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji kutoka Kituo cha Sheria na haki za Binadamu Bi. Imelda Urio akitoa mapendekezo kuhusu kudhibiti mauji na ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi katika mkutano ulioandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora uliowahusisha wadau mbalimbali jijini Dar es Salaam
6
Bw. Said Linze wa Baraza Kuu na Jumuiya na Taasisi za Kislam Tanzania akitoa maoni katika mkutano ulioandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ulikuwa unazungumzia namna ya kupanga mkakati wa kutoa elimu kwa umma katika kutokomeza tatizo la mauji na ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini jijini Dar es Salaam.
7
Wadau wa Mkutano wa kupanga mkakati wa namna ya kutoa elimu kwa umma katika kutokomeza tatizo la mauji na ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi ulioandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakiangalia moja ya filamu fupi iliyokuwa inaelezea matatizo yanayowakumba watu hao wenye ulemavu wa ngozi nchini.
8 9
Wadau wa Mkutano wa kupanga mkakati wa namna ya kutoa elimu kwa umma katika kutokomeza tatizo la mauji na ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi ulioandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakiangalia moja ya filamu fupi wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wadau katika mkutano huo jijini Dar es Salaam.

                                                                           (Picha na Lorietha Laurence-Maelezo)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni