Rais wa Tunisia ameapa kupambana na
ugaidi bila ya huruma, kufuatia shambulio la kutumia silaha kwenye
Jumba la Makumbusho la Bardo katika Jiji la Tunis lililouwa watu 19.
Watalii 17 wameuwawa kwenye
shambulio hilo, wakiwemo wageni kutoka nchi za Japan, Italia,
Colombia, Australia, Ufaransa, Poland pamoja na Hispania.
Watunisia wawili, mmoja wao akiwa ni
afisa polisi, nao wameuwawa katika shambulio hilo lililofanyika jana.
Vikosi vya usalama vya Tunisia
vimewauwa wahusika wawili wa shambulio hilo na wanaendelea kuwatafuta
washirika wao.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni