Wizara ya Ulinzi ya Marekani
imethibitisha kuwa imemuua kiongozi wa al-Shabab, aitwae Adan Garar.
Pentagon imesema kiongozi huyo
ameuwawa kwa kutumia bomu lililorushwa na ndege inayoruka bila rubani
katika eneo la kusini mwa Somali Ijumaa iliyopita.
Garar anadaiwa kuhusika na tukio la
shambulio la kwenye jengo la Westgate mnamo mwaka 2013 Jijini
Nairobi na kuua watu wapatao 67.
Marekani inaamini kuwa Garar alikuwa
anasimamia operesheni zenye kulenga raia wa Marekani pamoja na wa
nchi zingine za magharibi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni