Wananchi
wa Singapore, leo wanashiriki mazishi ya aliyekuwa baba wa taifa na
kiongozi aliyeleta mageuzi ya kiuchumi ya nchi hiyo, hayati Lee Kuan
Yew.
Maelfu
ya watu wanaonekana wakiwa wamejipanga katika misururu mirefu
kushiriki mazishi hayo huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha.
Mwili
wa kiongozi huyo utatolewa kwenye ukumbi wa bunge ambako viongozi
mbali mbali wa kimataifa walipata fursa ya kuuaga, na kutembezwa
katika mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo kabla ya kwenda kuzikwa kwenye
mazishi ya kifamilia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni