Upigaji
kura katika kinyang'anyiro cha kuwani kiti cha urais umeendelea kwa
siku ya pili leo nchini Nigeria kutokana na matatizo ya kiufundi
yaliyopelekea uchaguzi huo kuchelewa katika baadhi ya maeneo.
Katika
uchaguzi huo, rais Goodluck Jonathan anawania kuchaguliwa kwa awamu
ya pili, huku akikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa aliyekuwa
kiongozi wa kijeshi Muhammadu Buhari.
Hata
hivyo zoezi hilo limeingia dosari baada ya takribani watu 20 kuuawa
huko jimbo la Gombe katika mashambulizi yanahisiwa kufanywa na
wapiganaji wa kundi la kigaidi la Boko Haram.
Bibi akiweka kidole kwenye kifaa cha kumtambua mpigakura
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni