Na, Mwandishi Wetu
Maandamano ya wananchi ya ukosefu wa
maji maeneo mbalimbali Jijini Arusha, yametikisa jiji hilo jana, baada
ya wananchi wa kata ya Moshono kuandamana hadi ofisi ya mamlaka ya
maji safi na taka Jijini Arusha (AUWSA), wakidai hawajapata maji kwa
zaidi ya wiki
mbili.
Maandamano hayo yaliyokuwa ya
kisayansi, kwa kutumia usafiri wa magari na kuingia hadi ofisi za
mamlaka hiyo, yaliwashutukiza maafisa wa Mamlaka hiyo pamoja na
wajumbe wa bodi
waliokuwa kwenye kikao cha kujadili
maadhimisho ya wiki ya maji, kilichoanza juzi na kilele chake kufikai
Machi 21 mwaka huu.
Maandamano hayo yamesababisha kikao
cha bodi kuahirishwa kwa muda, na Mwenyekiti wa bodi hiyo Felix Mrema
na mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na taka jijini Arusha,AUWSA,
Mhandisi Lucy Koye ,na wajumbe walilizamika kukutana na wananchi hao
kutoa ufafanuzi.
Mkurugenzi wa AUWSA , Mhandis ,Koye,
alisema maji yaliyopo kwenye chanzo hicho hayatoshelezi mahitaji ya
wananchi, hivyo mamlaka inatafuta vyanzo
vingine.
Ameongeza eneo hilo lenye chanzo
hicho cha maji halimilikiwi na AUWSA, ndio maana maji yanayozalisha
kutoka kwenye eneo hilo ni machache .
Naye Mwenyekiti wa bodi ya mamlaka
hiyo, Felix Mrema, amewaambia wananchi hao kuwa kisima hicho hakina
maji ya kutosha na pia eneo hilo halijamilikishwa kwa mamlaka hiyo.
Kwa upande wake Mbunge wa Arusha
Mjini Godbless Lema, amesema hakwenda kuungana na wananchi hao kwa
ajili ya siasa, bali amefika kusaidiana kutafuta ufumbuzi na kuwataka
wananchi kuondoa vikwazo vilivyopo, ili kuiwezesha AUWSA ,kuzalisha
maji.
Katika hatua nyingine wajumbe wa
bodi, mbunge na wananchi walitembelea chanzo cha maji kilichopo
Moshono na kisima (tanki) ambapo wameteua kamati ya watu 15, ambayo
itafuatilia upatikanaji wa maji katika eneo hilo la Moshono.
Akitoa maelezo, mhandisi wa maji,
Gasto Francis Mkawe, amesema tatizo lililopo ni mgao wa umeme ambao
unaathiri uzalishaji wa maji .
Amesema tatizo la maji ni kubwa
jijini Arusha, ambapo mahitaji kwa siku ni lita milioni 100 lakini
kutokana na mgao wa umeme uzalishaji umeshuka hadi kufikia lita
milioni 45 tu ambapo katika eneo la Moshono pekee, uzalishaji
umeshuka hadi kufikia galoni 100.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni