Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akionyeshwa kisima cha maji kinachotumiwa na vikundi vya vijana vya Vijana Tujiajiri na Miti ni Uhai Wilayani Nzega ambavyo vilipewa msaada na NHC wa mashine za kufyatua matofali yanayofungamana.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akiangalia namna mchanga wa kufyatulia matofali yanayofungamana unavyoandaliwa alipotembelea vikundi vya vijana vya Vijana Tujiajiri na Miti ni Uhai Wilayani Nzega jana. Vikundi hivi vilipewa mashine ya kufyatulia matofali na NHC kama sehemu ya kusaidia vijana ajira nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akitoa mchango wa kununua sementi kwa vikundi vya vijana vya Vijana Tujiajiri na Miti ni Uhai Wilayani Nzega ambavyo vilipewa msaada na NHC wa mashine za kufyatua matofali yanayofungamana.Vikundi hivyo sasa vinapata kazi za kuwatengenezea wateja mbalimbali matofali hayo na hivyo kuwa na ajira endelevu.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu na ujumbe wake wakionyesha na Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo ramani yaeneo lililopewa NHC ili kujenga nyumba za gharama nafuu Wilayani Nzega.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akipewa maelezo na Msimamizi wa mradi wa nyumba za gharama nafuu Bw. Mwikuka juu ya hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa nyumba 50 zinazojengwa na NHC eneo la Zongomela Wilayani Kahama.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akisalimiana na mafundi ujenzi alipotembelea mradi wa nyumba 50 za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Zongomela Wilayani Kahama.
Mkurugenzi wa Usimamaizi wa Mikoa na Utawala Bw. Raymond Mndolwa akishiriki ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Kahama mara baada ya Uongozi wa Shirika kutembelea mradi huo jana.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akisisitiza umuhimu wa kupunguza gharama za ujenzi wa nyumba za gharama nafuu unaofanywa na NHC ili kuwawezesha wananchi wengi kumudu bei ya nyumba hizo alipotembelea nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC Wilayani Kahama ili kuukagua mradi huo jana.
Mkurugenzi wa redio Kahama FM Bw. Marco Mipawa akimpa maelezo Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu alipotembelea studio hizo ili kufafanua namna wananchi wanavyoweza kununua nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC eneo la Zongomela Wilayani Kahama jana. Ujenzi wa nyumba hizo utakamilika mwezi Agosti mwaka huu na kuuzwa kwa wananchi.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akiongea na wafanyakazi wa NHC Mkoa wa Shinyanga(hawapo pichani) akisisitiza watende kazi zao kwa mtizamo wa kibiashara na kuongeza tija na kwamba hatasita kumuondoa kazini mtumishi yeyote wa Shirika ambaye atashindwa kufikia malengo aliyopewa.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akibatilisha eneo la kujenga nyumba ya biashara mjini Singida kwa Msimamizi wa mradi huo kutoka kampuni ya B.H Ladwa inayojenga jengo hilo. Kwa sasa jengo hilo litajengwa mbele ya jengo la Singida Motel ili kuweza kuvutia wafanyabiashara watakaopanga katika jengo
Jumatatu, 23 Machi 2015
ZIARA YA MKURUGENZI MKUU WA NHC, NEHEMIA MCHECHU KATIKA MIKOA YA SINGIDA, TABORA NA SHINYANGA
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni